Misaada yasambazwa Nepal

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Misaada yawasili kwa waathiriwa

Misaada ya kibinadamu imeanza kuwasili katika wilaya ya Dhading, karibu na kitovu cha tetemeko la ardhi lililotokea nchini Nepal na kusababisha vifo vya zaidi ya watu elfu tano.

Lakini pia vijiji vingi nchini humo bado havijafikiwa na misaada.

Katika mji mkuu Kathmandu, mvua kubwa iliyonyesha kote usiku wa kuamkia leo Jumatano, ilitatiza pakubwa shughuli za uokoaji.

Maelfu ya watu wanajaribu kuondoka kwenye mji huo mkuu na kukimbilia vijijini muao ili kuwatafuta jamaa zao.

Siku ya Jumanne, wakwea milima wote waliokuwa wamekwama juu ya mlima Everest waliondolewa huku serikali ikisitisha shughuli zote za kuukwea mlima huo.