Manusura waendelea kutafutwa Nepal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waokoaji wakitafuta manusura Nepal

Makundi ya uokoaji yamefanya kazi usiku kucha nchini Nepal, kwa matumaini ya kupata manusura zaidi wakiwa hai, baada ya mkasa wa tetemeko baya la ardhi lililokumba taifa hilo siku ya Jumamosi.

Mwaandishi habari wa BBC aliyeko mjini Kathmandu, anasema kuwa ni harakati za kukomboa wakati, ili kupata watu ambao bado wangali hai.

Maelfu ya watu wangali wanakesha nje usiku kwa siku ya nne sasa tangu tetemeko hilo lilipotokea, wakihofia kutokea mitetemeko zaidi au kwa sababu nyumba zao zilibomolewa.

Kufikia sasa kuna vijiji ambavyo bado havijafikiwa na makundi ya uokoaji.