Raia wa Burundi watafuta hifadhi ubalozi wa Marekani
Huwezi kusikiliza tena

Raia watafuta hifadhi ya kibalozi

Nchini Burundi kuna taarifa kuwa raia takribani elfu moja wa Burundi wengi wao wakiwa ni wanafunzi wemekimbilia katika ubalozi wa marekani uliopo katika mji wa Bujumbura na kuomba hifadhi wakiohofia usalama wao.

Kumekuwa na vurugu na maandaamano kwa takriban siku ya tano sasa, ya kumpinga Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kugombea kwa muhula mwingine wa tatu baada ya chama chake kumteua kuwa mgombea urais kupitia chama hicho.

Hali imeendelea kuwa tete kwa siku ya tano sasa na haijulikani ni lini amani itarejea.

Hapo jana serikali ilifunga vyuo vikuu katika mji mkuu wa Bujumbura na Hawa ni baadhi ya waandamanaji katika viunga vya Musaga walipokuwa wakiandamana hapo jana.

Regina Mziwanda amezungumza na Ismail Misigaro aliyepo Bujumbura na Kwanza alimuuliza juu ya taarifa hizi kuwa raia wa Burundi zaidi ya elfu moja wengi wao wakiwa ni wanafunzi wamekimbilia katika ubalozi wa Marekani zikoje?