Floyd Mayweather amshinda Pacquiao

Haki miliki ya picha AP
Image caption Pacquiao na Mayweather

Bondia wa Marekani Floyd Mayweather ameshinda pigano lililosubiri kwa wingi katika miongo kadhaa.

Haki miliki ya picha
Image caption Mayweather amshinda Pacquiao

Bondia huyo ambaye hajashindwa alimshinda mpinzani wake raia wa Ufilipino Manny Pacquiao kwa wingi wa pointi.

Haki miliki ya picha
Image caption Pacquiao akimpiga makonde mayweather

Mashabiki wengi waliojaa katika ukumbi wa MGM Grand Garden Arena mjini Las Vegas walimzoma mara kwa mara Mayweather.

Haki miliki ya picha
Image caption Mayweather ashinda kwa wingi wa pointi

Kote duniani wateja millioni 3 walilipa kuliona pigano hilo ambalo ndio pigano lililovutia kitita kikubwa cha fedha katika historia ya ndondi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mayweather

Tiketi nyingi za pigano hilo ziliuzwa katika bei ya makumi ya maelfu ya dola.