Misaada:Nepal yatakiwa kulegeza sheria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Misaada Nepal

Umoja wa Mataifa umeishauri serikali ya Nepal kulegeza vizuizi vya ushuru ambavyo inasema vinatatiza utoaji wa misaada kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi la wiki iliyopita.

Mkuu wa huduma za kibinadamu wa umoja wa mataifa Baroness Amos alisema kuwa Nepal ina jukumu la kuharakisha kusafirishwa kwa misaada wakati kunapotokea janga

Nepal inasisitiza kuwa ni lazima ikague misaada yote ya dharura itakayowasili katika uwanja wa ndege mjini Kathmandu

Watu wengi maeneo ya mbali bado hawajapata misaada yoyote.

Takriban watu 7000 wameripotiwa kuaga dunia kwenye janga hilo.