Maandamano yazimwa,Israel

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu

Polisi nchini Israel wakiwa juu ya Farasi wamekabiliana na waandamanaji kutoka makundi ya Wayahudi wenye asili ya Ethiopia ambao wanadai kubaguliwa na Polisi wa taifa hilo.

Katika maandamano hayo yalitokea Tel Aviv, Polisi walitumia mabomu ya machozi na maguruneti kuwatawanya mamia ya waandamanaji hao. Watu kadhaa wamejeruhiwa wakiwemo maafisa wa Polisi 20. Wayahudi wenye asili ya Ethiopia waliitisha maandamano kufuatia picha za video zilizosamabaa wiki iliyopita ambazo zinaonyesha askari wenye sare wenye asili ya Ethioppia wakiteswa na Polisi. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa wito kurejesha hali ya Amani na kuahidi kuwa polisi watafuatilia tuhuma hizo na kuzifanyia uchunguzi wa kina