IS yawaua raia 300 wa Yazidi nchini Iraq

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia wa Yazidi

Maafisa nchini Iraq wanasema kuwa wanamgambo wa islamic state wamewaua mamia ya watu wa yazidi waliokuwa wakiwazuilia eneo lililo kaskazini mwa nchi.

Makamu wa rais nchini Iraq Osama al-Nujifi ameyalaani mauaji hayo akiyataja kuwa ya kikatili

Taarifa zilisema kuwa hadi watu 300 waliuawa kwenye wilaya moja iliyo magharibi mwa mji wa Mosul siku ya ijumaa.

Wanamgambo wa islamic state walithibiti maeneo yaliyo kaskazini mwa Iraq kwa karibu mwaka mmoja uliopita ambapo waliwaua na kuwashika mateka maelfu ya watu wa Yazidi wakiwaita makafiri.