Netanyahu ashutumu ubaguzi Israeli

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Netanyahu

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameelezea mshangao wake binafsi kwa mwanajeshi wa Israeli wa asili ya Ethiopia ambaye alipigwa na polisi wa Israeli hali iliyosababisha kutokea kwa maandamano.

Bwana Netanyahu alimuambia Damas Fikadeh kuwa kitendo hicho hakikubaliki, na madabiliko yanahitaji kufanywa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maandamano Israel

Bwana Fikadeh alisema alitiwa moyo na matamshi yake waziri mkuu na ni wakati wa kumaliza ghasia za ubaguzi dhidi ya Waisraeli wa asili ya Ethiopia.

Wakati wa ghasi hizo za siku ya jumamosi usiku mjini Tel Aviv takriban watu 50 walijeruhiwa.

Image caption Waandamanaji Israel

Wakati huohuo rais wa Israeli Reuven Rivlin amesema kuwa ni makosa jinsi Israeli inavyowafanyia wayahudi wenye asili ya Ethiopia.

Akizungumza baada ya maandamano yenye ghasia mjini Tel Aviv bwana Rivlin alisema kuwa kidonda kilicho wazi kimeonekana nchini Israeli , lakini ghasia sio suluhu.

Image caption maandamno israel

Zaidi ya watu 50 walijeruhiwa siku ya Jumapili wakati polisi walitumia vituo machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji.