Raia wa Israel kutoka Ethiopia walalama

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia wa Israel wenye mizizi yao nchini Ethiopia wamedai kubaguliwa nchini humo

Polisi wa Israeli waliokuwa wakitumia farasi, walikabiliana vikali na waandamanaji, wakati wa makabiliano katikati mwa mji wa Tel Aviv.

Walitumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za mipira, ili kuwatawanya waandamanaji wenye asili ya Waisraeli- waitheopia, wanaopinga unyanyasaji wa polisi wanaowabagua.

Zaidi ya watu hamsini wamejeruhiwa na polisi.

Waziri mkuu, Benjamin Netanyahu, ameomba kuwepo kwa hali ya utulivu, huku akisema kuwa madai yote ya ubaguzi wa polisi yatachunguzwa.