Nepal:Watoaji misaada watakiwa kuondoka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nepal yapata misaada

Nepal imewataka watoa huduma za misaada ya kigeni kwenye mji mkuu Kathmandu na maeneo yanayozunguka mji huo kurudi makwao ikisema kuwa asiliamia kubwa ya kazi imekamilika.

Serikali inasema kuwa oparesheni za uokoaji zilizosalia maeneo ya mbali ya vijijini zinaweza kufanywa na polisi na jeshi.

Tangu nchi hiyo ikumbwe na tetemeko la ardhi siku 9 zilizopita zaidi ya watoa huduma 4000 kote duniani wamekuwa wakisadia kutoa misaada na oparesheni za ukoaji.