Vikosi vya Syria vyalaumiwa kwa uhalifu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Syria

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limevilaumu vikosi vya serikali ya Syria kwa kuendelea kutekeleza vitendo vya uhalifu wa kivita kila siku kwenye mji wa Allepo, kwa kushambulia vibaya maeneo yanayothibitiwa na waasi.

Amnesty imechapisha ushahidi wa ahalifu ambao umesababishwa na mabomu ya mapipa ambayo yamedondoshwa kwenye mahospitali , misikitini na shuleni.

Amnesty inasema kuwa mabomu ya mapipa yaliwaua zaidi ya watu 3000 mjini Allepo mwaka uliopita.

Ripoti pia inasema kuwa waasi hao nao wameendesha uhalifu wa kivita.