Jaji wa korti ya kikatiba atoroka Burundi

Haki miliki ya picha
Image caption burundi

Makamu wa rais wa mahakama ya katiba nchini Burundi anaripotiwa kuondoka nchini humo kabla ya kutolewa kwa uamuzi iwapo ni halali rais kugombea muhula wa tatu.

Jaji Sylvere Nimpagaritse aliliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa mahakama ilikuwa imekabiliwa na shinikizo vikiwemo vitisho vya kuuawa ili kuweza kuidhinisha hatua ya rais Pierre Nkurunzia kuweza kusallia madarakani.

Hatua hiyo imesababisha kushuhudiwa kwa maandamano yenye ghasia nchini Burundi.