Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Huwezi kusikiliza tena

Pierre Nkurunziza ruksa kuwania urais

Mahakama ya kikatiba nchini Burundi imemruhusu rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.Kulingana na vituo vya redio nchini humo,Jaji wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi .

Hapo Jana makamu wa mahakama hiyo Jaji Sylvere Nimpagaritse ,alilitoroka taifa hilo akidai kuwa walikuwa wakishinikizwa kutoa uamuzi utakaompendelea rais Nkurunziza.

Rwanda imethibitisha kuwa jaji huyo yuko mjini Kigali.Kufuatia hali hiyo mwandishi wetu wa Dar-Es-Salaam Regina Mziwanda alifanya mazungumzo na msemaji wa Rais wa Burundi Gervais Abayeho pamoja na mambo mengine,serikali ya Burundi imeuchukuliaje uamuzi wa mahakama?