John Kerry azuru mji wa Mogadishu

Haki miliki ya picha AP
Image caption John Kerry azuru Mogadishu

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amewasili katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo anakutana na rais Hassan Sheikh Mohamud,viongozi wa eneo la Afrika mashariki pamoja na mashirika ya kijamii.

Ni waziri wa kwanza wa kigeni kutoka Marekani kuutembelea mji huo.

Kerry hataondoka katika uwanja wa ndege wa mji huo unaolindwa sana.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais wa Somalia

Wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani inataka kutoa ujumbe kwa kundi la Alshabaab kwamba halipatii kisogo taifa la Somalia.

Marekani imetoa mamia ya madola nchini Somalia katika siku za hivi karibuni.

Ndege zisozokuwa na rubani za Marekani zimewaua viongozi kadhaa wa kundi la Alshabaab.