Wafghan 4 kunyongwa kwa mauaji

Image caption Waandamanaji wakipinga mauaji ya Farkhunda

Jaji wa Mahakama ya Afghan amewahukumu wanaume wanne adhabu ya kifo kwa kumuua kwa kumshambulia mwanamke mmoja mjini Kabul.

Mwanamke huyo anayeitwa Farkhunda alipigwa hadi kufa na kundi la watu wenye hasira baada ya kutuhumiwa kimakosa kuchoma kitabu cha Koran.

Mwili wake ulichomwa mwoto. Watu wengine 49 wanaendelea na kesi, wakiwemo polisi 19 wanaotuhumiwa kwa kushindwa kuingilia kati kumwokoa mwanamke huyo.

Mauaji hayo yalisababisha hasira kutoka maeneo mbali mbali duniani ambayo pia yalisababisha maandamano nchini Afghanistan kupinga jinsi mwanamke huyo alivyotendewa.