Wanne wafa katika maandamano Burundi

Haki miliki ya picha
Image caption Maandamano nchini Burundi

Watu wanne wamekufa na wengine tisa kujeruhiwa katika maandamano yanayoendelea kupamba moto nchini Burundi kupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Mwandishi wa BBC aliyepo mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura anasema mamia ya watu wamejitokea kwenye maandamano hayo huku baadhi wakichoma moto baadhi ya vitu.

Siku ya jumanne Mahakama ya Katiba ilikubali kuwa Rais Nkurunziza anaweza kugombea urais ambapo ilisema ni halali yeye kuwania tena urais kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Katika hotuba yake siku ya jumatano Rais Nkurunziza alisema kama atachaguliwa tena kuongoza nchi hiyo, muhula huu utakuwa wa mwisho kwake kuwa madarakani.