Chama cha David Cameron chashinda uchaguzi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri huyo mkuu hata hivyo anawaomba wafuasi wake wasubiri hadi matokeo kamili yatangazwe

Waziri mkuu David Cameron amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Uingereza hiyo jana.

Chama chake cha Conservative kimejipatia viti 330 huku kile cha leba kikijipatia 232.

Cameron amesema kuwa anapania kuendelea kuiongoza Uingereza ya pamoja .

Shirika La BBC lilikisia kuwa Cameron na Chama chake angepata ushindi wa maeneo bunge 329.

Chama cha Leba kimepata pigo kubwa huko Scotland kutoka kwa chama cha kitaifa cha Scotland National Party SNP .

Image caption Cameron na Conservatives washinda uchaguzi wa Uingereza

Licha ya Matokeo hayo Mazuri huko Scotland ambapo SNP ilisajili ushindi mkubwa wa majimbo 50 chama hicho hakikutamba katika maeneo ya England na Wales.

Chama cha The Liberal Democrats wanaelekea kusajili matokeo duni wakiwa tayari wameshinda viti vinane pekee.

Nyota wa chama hicho (Lib Dems) Vince Cable, Ed Davey na Danny Alexander wote wameshindwa katika uchaguzi huo.

BBC ilikuwa imebashiri kuwa Conservative watasajili ushindi katika maeneo bunge 329, Labour 233, the Lib Dems 8, SNP 56, Plaid Cymru 3, UKIP2, Greens 1 na vyama vyengine vidogo viti 19.