Iran yaiachilia huru meli ya mizigo

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Meli hiyo Maersk Tigris iliyoachiliwa huru na Iran

Iran imeachia meli ya mizigo iliyoikamata katika maeneo ya baharini huko Hormuz, juma lililopita.

Shirika la habari la Iran, linasema kuwa meli hiyo ya mizigo, inayomilikiwa na kampuni moja kutoka Denmark na kuandikishwa katika visiwa vya Marshall sasa iko huru kuondoka Iran.

Meli hiyo iitwayo Maersk Tigris -- ilipiga kona na kutia nanga katika bandari moja ya Ghuba iitwayo Bandar Abbas, kufuatia mzozano na kampuni moja ya Iran.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Manuari za kijeshi za Iran zilizoiteka meli ya mizigo huko Hormuz

Mahakama moja nchini Italia iliamuru kampuni ya Maersk kulipa faini ya dola milioni tatu u nusu.

Kisa hicho kiliibua taharuki ya usalama na kuilazimu manuari ya jeshi la Marekani kuamua kuipa usalama meli iliyokuwa na bendera ya Marekani

pamoja na kuwatuma wanajeshi wake wa majini kuchunguza nyendo za meli za kijeshi za Iran.