Chanjo ya Malaria yaonesha mafanikio Kenya

Haki miliki ya picha 3DMEDICAL.COM SCIENCE PHOTO LIBRARY
Image caption Chanjo ya Malaria yaonesha mafanikio Kenya

Majaribio ya chanjo dhidi ya malaria nchini Kenya yameonesha dalili nzuri ya mafanikio.

Wanasayansi watafiti kutoka Chuo kikuu cha Oxford Uingereza wamesajili asili mia 67% ya mafanikio katika majaribio ya chanjo hiyo kwa wakenya 121.

Utafiti huo ni wa pili wa haiba yake katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Haki miliki ya picha none
Image caption WHO inasema kuwa visa milioni 198 vya malaria viliripotiwa mwaka wa 2013 huku takriban watoto 584,000 wakipoteza maisha yao.

Majaribio ya chanjo nyengine tofauti pia yameonesha mafanikio katika kuwakinga watoto wachanga.

Takwimu zinaonesha kuwa watoto 1,300 wanakufa kila siku chini ya jangwa la Sahara kutokana na ugonjwa huo.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa visa milioni 198 vya malaria viliripotiwa mwaka wa 2013 huku takriban watoto 584,000 wakipoteza maisha yao.

Ajabu ni kuwa hakujakuwa na mafanikio makubwa kuhusu mbinu za kupambana na kirusi kinachosababisha malaria.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Virusi vya Malaria

''Plasmodium falciparum'' anayeishi katika mbu walioambukizwa.

Kimsingi watafiti hao wamegundua kuwepo kwa aina nne ya virusi.

Aidha haijabainika iwapo chanjo hiyo itakabiliana na aina zote nne za virusi.

Utafiti huo ambao umekuwa ukiwafuatilia wanaume 121 kwa majuma 8 umegundua kuwa idadi ya virusi vinapungua kwa thuluthi mbili.

Image caption Mbu aliyeambukizwa na virusi vya ''Plasmodium falciparum''

Watafiti hao wamegundua aina ya chanjo inayovamia kirusi ndani ya maini ya mgonjwa.

''Kiwango cha juu cha mafanikio kama tulivyoshuhudia hapa ni ishara nzuri ''.

''Tunachohitaji ni utafiti zaidi ili tuwanusuru mamilioni ya watoto wanaoathirika na Malaria''

Alisema Mtafiti mkuu Prof Adrian Hill.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kimsingi watafiti hao wamegundua kuwepo kwa aina nne ya virusi.

Hatua ya pili ya utafiti huu sasa unaelekea Burkina Faso ambapo utafiti utahusisha watoto.

Profesa Chris Drakeley, kwa upande wake alionya kuwa kunahaja kubwa ya tahadhari maanake huenda madawa haya yakafaa watu wazima ilhali watoto ndio wanaoathirika kwa kiwango kikubwa zaidi.

Hata hivyo Profesa Drakeley, anashauri kinga dhidi ya ugonjwa huu ni kulala ndani ya vyandarua vilivyotibiwa.