Thailand kufunga kambi za walanguzi

Haki miliki ya picha epa
Image caption Thailand kufunga kambi zinazotumiwa kuwalangua watu

Waziri mkuu wa Thailand Prayut Chan-o-cha, ameamrisha kuondolewa kwa kambi zinazotumiwa kuwalangua watu kinyume cha sheria katika kipindi cha chini ya siku kumi.

Hatua hiyo inafuatia kugunduliwa kwa zaidi ya maiti 30, ndani ya makaburi ya halaiki karibu na mpaka na Malaysia.

Maiti hizo zinaaminiwa kuwa za wahamiaji haramu kutoka nchini Mnyanmar na Bangladesh.

Image caption Makaburi ya karibu yaliyopatikana mwituni

Utawala nchini Thailand unasema kuwa polisi 50 wamehamishwa kwa kushukiwa kuhusika kwenye usafrishaji haramu wa binadamu tangu kupatikana kwa maiti hizo.

Wahamiaji wengi haramu wanadaiwa kuwa ni Waislamu wa jamii ya wa- Rohingya wanaotoroka mateso kutoka Myanmar, (awali ikifahamika kama Burma.)