Uingereza:Mbunge mchanga zaidi miaka 20

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mbunge mchanga wa SNP Mhairi Black

Wapiga kura nchini Scotland wamemchagua mwanafunzi wa chuo kikuu kuwa mbunge wao.

Bi Mhairi Black, alishinda kura za eneo bunge la Paisley and Renfrewshire South na kumbwaga kigogo wa chama cha Labour aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni bwana Douglas Alexander.

Mbali kuzua mjadala kwa kumbwaga kigogo wa chama cha Leba na kumaliza ukiritimba wa chama cha Leba Bi Black sasa ndiye Mwakilishi wa kwanza katika kipindi cha miaka 70 ambaye si mwanachama wa Leba.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mbunge mchanga zaidi Uingereza Mhairi Black

Aidha ameweka rekodi ya kuwa mbunge mwenye umri mdogo zaidi nchini Uingereza tangu karne ya 17.

Black ana umri wa miaka 20 pekee.

Bi Black anamfuata mbunge mwengine aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo ya 1667, bwana Christopher Moncktook.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Black ana umri wa miaka 20 pekee

Bwana Moncktook alikabidhiwa uongozi akiwa na umri wa miaka 13 .

Wakati huo hata hivyo mamlaka yalinasibishwa na hivyo haikutambuliwa kama uchaguzi haswa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bi Black alipotangazwa mshindi akiwa na mpinzani wake Bw Alexander

Lakini Bi Black alihakikisha jina lake linaingia katika kumbukumbu za historia kwa kuvunja rekodi hiyo iliyowekwa miaka 350 iliyopita alipozoa kura 23,548 dhidi ya 17,864 za Alexander.

Majuzi hata hivyo mbunge aliyekuwa akitambuliwa kama mchanga zaidi kuchaguliwa alikuwa ni Charles Kennedy wa chama cha Liberal Democrat aliyechaguliwa akiwa na umri wa mia 23.