MSF lafunga hospitali yake Sudan Kusini

Haki miliki ya picha MSF
Image caption MSF

Shirika la madaktari wasio na mipaka ,Medicins Sans Frontiers MSF limesema kuwa limewandoa wafanyikazi wake katika jimbo la Unity state nchini Sudan Kusini kufuatia kuzuka kwa vita vipya kati ya waasi na vikosi

vy serikali.Shirika hilo linasema kuwa limelazimika kufunga hospitali yake muhimu ya Leer ikiwa ndio ya kipekee katika jimbo hilo.

Leer ndio nyumbani kwa kiongozi wa waasi Riek Machar.

Hospitali hiyo ilishambuliwa mwaka uliopita .

Afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa anayesimamia maswala ya binaadamu nchini humo Tobby Lanzer ameyataka makundi pinzani kuruhusu misaada kuingia katika eneo hilo.

Hadi raia laki moja wamewachwa bila makao katika jimbo la Unity state katika kipindi cha juma moja.