Urusi yasherehekea ushindi dhidi ya Nazi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Urusi.

Waride kubwa la kijeshi mjini moscow tangu kuvunjika kwa Muungano wa Usovieti linaanza muda mfupi unaokuja lakini viongozi wa mataifa mengi ya magharibi hawatahudhuria.

Rais wa Urusi Vladimir Putin atakuwepo wakati maelfu ya wanajeshi watatembea eneo la Red Square kuadhimisha miaka 70 ya kuushinda utawala wa kinazi wa Ujerumani wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.

Marekani na viongozi wengi wa ulaya wamesusia sherehe hizo kupinga kuhusika kwa Urusi kweye mzozo ulio nchini ukrain.