NATO yataka suluhu Macedonia

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Polisi wa Macedonia

Viongozi wakuu wa vikosi vya shirika la kujihami kwa mataifa ya magharibi NATO wametoa wito wa kuzuia ghasia zinazoendelea Macedonia kufuatia ghasia zilizozuka mwishoni mwa wiki.

Zaidi ya watu ishirini pamoja na polisi nan a watu wengine kumi na wawili wenye silaha walipoteza maisha wakati wa mapigano upande wa Kaskazini wa mji wa Kumanovo, ulioko karibu na Macedonia mpakani mwa Kosovo na Serbia.

Katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, ametaka kuwe na uchunguzi huru na wa wazi juu wa tukio hilo.

Mamlaka za Macedonia zimesema kwamba wapiganaji wa koo la Albania kutoka Kosovo walijipenyeza Kumanovo wakiwa na mipango ya mashambulio katika nchi nzima.

Lakini wanaharakati wa upinzani wanatuhumu ghasia hizo kama mpango wa serikali ambayo inakabiliwa na uvunjifu wa sheria ,wizi wa kura na ufisadi.