Waasi wakubali kusitisha vita Yemen

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Yemen

Wanajeshi waasi nchini Yemen ambao waliwasaidia waasi wa Houthi kudhiditi maeneo makubwa ya nchi hiyo wamekubali usitishwaji wa mapigano kwa siku tano uliopendekezwa na saudi Arabia.

Msemaji wao kanali Sharaf Luqman anasema kuwa usitishwaji huo wa mapigano utaanza siku ya jumanne.

Lakini haijulikani iwapo anazunguzma kwa niaba ya waasi wote au la.

Vikosi vinavyoongozwa na Saudi Arabia vimeendesha mashambulizi kwenye mjii mkuu Yemen sanaa vikilenga nyumba ya rais wa zamani Ali Abdullah Saleh.