Je,mazingira huchangia kumpata jaji anayefaa?

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mahakama nchini japan

Waziri wa haki nchini Misri amezua hisia kali katika mitandao ya kijamii baada ya kusema kuwa mwana wa muokota uchafu hawezi kuwa jaji.

Katika mahojiano na runinga siku ya jumapili,Mahfouz Saber amesema kuwa kwa heshima yote kwa waokota uchafu ,jaji anayetarajiwa anafaa kutoka katika mazingira ya heshima.

Tamko hilo limezua hisia kali nchini humo huku maelfu ya ujumbe wa twitter ukitaka afutwe kazi.

Aliyekuwa makamu wa rais Mohammed El Baradei amesema kuwa iwapo hakuna haki katika taifa basi hakuna linalosalia.