Mchezaji kugharamia hasara ya bao lake

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Mchezaji kandanda ameahidi kulipia hasara iliyosababishwa na shabiki wake alipofunga bao.

Mchezaji kandanda ameahidi kulipia hasara iliyosababishwa na shabiki wake alipofunga bao.

Shabiki huyo sugu Ross Morgan, 25, alikuwa akitizama mechi kati ya Ipswich na Norwich jumamosi iliyopita wakati huo timu yake ikiwa nyuma kwa bao moja.

Hata hivyo anasema alishikwa na wazimu akaruka juu na kupiga ngumi dari ya nyumba yake ikatoboka baada ya Paul Anderson kufunga bao la kusawazisha.

Image caption Morgan, alisisimka na akagonga dari ya nyumba yake akitizama mechi ya Ipswich

Morgan aliipiga picha shimo hilo na akaiweka kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

Mashabiki wenza waliisambaza na ikamfikia Anderson ambaye ilimgusa na akajitolea kugharamia hasara aliyosababisha.

Image caption Anderson alijitolea kufidia gharama ya ufundi ilikuirejesha nyumba yake katika hali nzuri.

Anderson alijitolea kufidia gharama ya ufundi ilikuirejesha nyumba yake katika hali nzuri.

Mchezaji huyo wa Ipswich aliwatamausha mashabiki waliokuwa wakifuatilia mazungumzo yao kwa ukarimu wake.

Image caption Morgan, aliachwa kinywa wazi na ukarimu wa Anderson.

Morgan, aliachwa kinywa wazi na ukarimu wa Anderson.

Kwa sasa shabiki huyo sugu anapania kutizama mechi ya marudiano kati ya Ipswich na Norwich katika uwanja wa Wembley siku ya jumamosi.