Wakimbizi taabani Thailand

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakimbizi waliokamatwa Thailand

Maelfu ya wakimbizi kutoka Bangladeshi na Myanmar wametelekezwa karibu na ufuo wa Thailand kufuatia masharti makali yaliyowekwa majuzi.

Shirika la kimataifa linalishoghulikia maswala ya wahamiaji IOM, limesema kuwa hatua ya hivi punde ya serikali kuvunjilia mbali kambi za wakimbizi na

kuwakamata maharamia wanaolangua watu imewaogopesha wakimbizi hao wanaotoroka mateso katika mataifa hayo kushindwa kufika ufukweni.

Msemaji wa shirika hilo ameiambia BBC kuwa watu hao wa tabaka la Rohingya wameshindwa kuingia Thailand na hivyo kusalia wakielea baharini wasijue cha kufanya.

Hata hivyo polisi nchini humo wanasema kuwa zaidi ya wakimbizi haramu elfu moja waliwasili nchini humo katika kipindi cha siku chache zilizopita.

Aidha Polisi wanadai kuwa wakimbizi hao waliwasili kupitia ufukwe wa Langkawi ulioko Kaskazini Mashariki mwa kisiwa hicho.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Serikali ilitangaza vita dhidi ya walanguzi wa watu baada ya kupatikana kwa makaburi ya wahamiaji

Mapema leo duru za polisi zimedokeza kuwa wakimbizi wengine elfu moja wamewasili Aceh wakishukiwa kuwa ni sehemu ya jamii ya Rohingyas wanaotoroka mateso kwao.

Wakimbizi wengine 600 ambao pia wanaaminiwa kutoka jamii ya Rohingya walishekwa na utawala wa indonesia siku ya jumapili.

Serikali ya Thailand iliamua kukaza kamba na kutangaza vita dhidi ya makundi yanayowalangua wanadamu baada ya kugundua makaburi thelathini ya karibu.