Raia wa Burundi wakiwa katika moja ya mitaa ya nchi hiyo
Huwezi kusikiliza tena

Raia wa Burundi watoa ya moyoni

Marais Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana leo jijini Dar Es Salaam kujadili mgogoro wa kisiasa unaendelea nchini Burundi.

Mkutano huo utakuwa chini uenyekiti wa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete aliyeuitisha baada ya ujumbe wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Jumuiya hiyo kwenda Bujumbura nchini Burundi wiki iliyopita.

Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, kusikiliza hoja za viongozi wenzake.

Lakini Je nao raia wa Burundi wana maoni gani kuhusu mkutano huo wa marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaoanza leo nchini Tanzania?