Kanye atunukiwa shahada ya heshima Chicago

Image caption Dr Kanye West ?Kanye atunukiwa shahada ya Heshima Chicago

Baada ya kuacha masomo yake akiwa na miaka 20 hata ikamchochea kuipa jina albamu yake ya kwanza ''The College Dropout'' tafsiri ya aliyeacha chuo

hatimaye Msanii wa mziki wa kufoka Kanye West amehitimu.

Kanye West ametunukiwa shahada ya heshima na taasisi ya Sanaa ya chuo kikuu cha Chicago.

Hili linamaanisha kuwa sasa West atafahamika kiheshima kama dakta Kanye West.

Chuo hicho kimemtunuku heshima hiyo kwa mchango wake katika sanaa ya muziki wa kufoka ambapo ''West amejijengea sifa kote duniani bila ya utunzi wa muziki unaombatana na sera kamili ya muziki''.

West aliwashukuru kwa heshima hiyo.

''kwa hakika ni jambo la kiheshima sana kwenu kunitunuku''

Image caption Dr Kanye West ?Kanye atunukiwa shahada ya Heshima Chicago

''sio kitu cha kupuuza kwa kweli ,kwa sasa hata mwili wangu unatetemeka kwa sababu ya furaha na unyenyekevu mbele yenu''

''Kwa hakikika kuimba muziki sio kitu rahisi lakini ukishaimba nyimbo zako kisha uzawadiwe kama mlivyonifanyia hii leo,kwa hakika inasafisha moyo''alisema Dakta West

West aliyejitambulisha kama mwanamuziki wa ''POP'' Alisema kuwa dunia ndio hadhira yake na kuwa umma unapaswa kuwajibikia na kujivunia misimamo yao.

Chuo hicho kilichukua hatua ya kumtunuku shahada hiyo baada ya kubaini kuwa aliwahi kukiri katika mahojiano kuwa alikuwa anatamani sana kusoma huko kabla hajabobea katika fanii ya muziki.