Hofu yazuka kuhusu hali ya wakimbizi Thai

Haki miliki ya picha reuters
Image caption Hofu yazuka kuhusu hali ya wakimbizi Thai

Hofu inazidi kuibuka kwa wahamiaji 350 wa Asia, wakiwemo zaidi ya watoto themanini, ambao wamekwama baharini na hawajapata chakula wala maji kwa siku nne sasa.

Kundi moja la utoaji msaada ambao linawasiliana na wahamiaji hao walioko kwenye mashua baharini, limesema kuwa baadhi yao wameanza kuugua.

Wahamiaji hao wengi kutoka kwa kabila dogo la rohingya wanaotoka nchini Myanmar, wanasema kuwa waliachwa baharini na wafanyikazi wa chombo hicho yapata siku ya jumapili.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wahamiaji waliokamatwa na maafisa wa usalama Thailand

Eneo hasa walikoachwa bado haijajulikana.

Inakisiwa kuwa maelfu ya wahamiaji elfu moja kutoka Myanmar na Bangladesh wamekwama baharini na kushindwa kufika katika nchi kavu nchini

Thailand tangu utawala nchini humo ulipobuni sheria kali dhidi ya mitandao ya walanguzi wa watu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waislamu wazika miili ya waislamu waliopatikana wameuawa mwituni

Serikali ya Thailand iliweka sheria mpya ya kupambana na walanguzi hao wa watu baada ya kugundua miili ya takriban wahamiaji 30 katika makaburi ya karibu mwituni.

Inakisiwa kuwa watu hao waliuawa baada ya kutofautiana na walanguzi waliokuwa wamewaweka katika kambi zao za siri.