Utafiti:Salamu zaweza kutabiri Kiharusi

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Wapinzani wao hata hivyo wanadai kuwa utafiti huu sio kamilifu

Je unakumbuka wale mabibi wanaotangaza huduma za kusoma mkono na kisha kutabiri maisha yako ya baadaye ?

Sasa kuna utafiti mpya unaosema kuwa hali ya afya ya mtu inaweza kubainika kulingana na udhabiti wa salamu zake.

Kulingana na utafiti huo uliochapishwa katika gazeti la maswala ya utabibu The Lancet, udhabiti wa salamu unaweza kuonesha dalili za mapema za ugonjwa wa kiharusi na mshtuko wa moyo.

Utafiti huo uliohusisha zaidi ya watu laki moja na arobaini (140,000) katika mataifa 14 kote duniani unaonesha kuwa udhabiti wa salamu unafifia kadri umri wa mja unavyoongezeka na kuwa salamu za nguvu zinaashiria afya nzuri.

Kwa sasa utabiri wa Kiharusi ama mshtuko wa moyo hutegemea kwa kiwango kikubwa msukomo na kasi ya damu ya mgonjwa.

Hata hivyo watafiti wenza wametaka tahadhari zaidi ichukuliwe kabla ya kutumia utafiti huo kama njia ya kwanza ya madaktari kubaini hatari ya kukabiliwa na mshtuko wa moyo ama kiharusi.

Kulingana na utafiti huo wanawake wenye umri wa kati ya maika 25 wananguvu za kilo 34, Lakini uzito huo huwa unafifia anapotimiza miaka 70 atanatarajiwa kuwa na mshiko wa kilo 24.

Haki miliki ya picha spl
Image caption Utafiti mpya unaonesha kuwa hali ya afya ya mtu inaweza kubainika kulingana na udhabiti wa salamu zake

Aidha takwimu za wanaume katika umri huohuo ni kilo 54 na 38 mtawalia.

Kulingana na utafiti huo iwapo udhabiti wa mashiko ya mtu unapungua kwa takriban kilo 5% basi uwezekano wake kuaga dunia mapema huongezeka kwa takriban asilimia 16%.

Aidha takwimu hizo zinamaanisha kuwa uwezekano wa kukumbwa na mshtuko wa moyo huongezeka kwa asilimia 17% huku uwezekano wa kukumbwa na kiharusi unaongezeka kwa asilimia 9%

Madaktari kwa sasa wanadadisi hali ya afya ya mtu kwa kuchukua habari kuhusu umri wake ,iwapo ni mvutaji sigara au la, kwa kupima kiwango cha mafuta mwilini mbali na kupima kasi ya damu.

Aidha madaktari pia huwa wanawauliza madaktari iwapo wanashida yeyote ya kifamilia na kama kuna mtu yeyote katika familia yao ameathirika na mshtuko wa roho ama kuugua ugonjwa wa shinikizo la damu.

Image caption Wapinzani hata hivyo wanataka utafiti zaidi kufanyika

Daktari mkuu Darryl Leong, wa chuo kikuu cha McMaster kilichoko Canada, alipigia upatu utafiti huu akidai kuwa itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza gharama ya matibabu haswa katika mataifa yanayoendelea.

Wapinzani wao hata hivyo wanadai kuwa utafiti huu sio kamilifu.

Dakta Doireann Maddock,wa wakfu wa moyo nchini uingereza alisema kuwa kuna haja kubwa ya utafiti zaidi katika kitengo hicho cha maradhi ya moyo.