Jehi la Indonesia lawamani

Image caption Wanawake walioko jeshini nchini Indonesia

Kikundi kimoja cha wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu nchini Indonesia ,kimetoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuacha mara moja zoezi la kukagua bikira za wanawake wanaotaka kujiunga na majeshi ya nchi hiyo.

Shirika hilo la kutetea haki za binaadamu limesema kwamba wanawake wanaotafuta kuajiriwa jeshini wamelalama juu ya kuwajibika kufanyiwa uchunguzi wa ndani zaidi ya maungo yao ili kuhakiki bikira kama zingalipo.

Nalo jeshi la Indonesia limetetea vipimo hivyo,kwa kusema kuwa vinasaidia kugundua mapema wanawake wenye tabia mbaya wanaotaka kujiunga na majeshi yao.

Polisi na jeshi nchini humo mwaka wa jana walikabiliwa na upinzani baada ya kuwa sheria kandamizi ya kuwalazimisha wanawake waombao ajira kupitia uchunguzi huo endapo kweli wana maanisha kuzihitaji ajira hizo.