Is yauharibu mji wa Palmyra,Syria

Image caption Mji huo wa Palmyra ulioharibiwa vibaya

Wakuu wa mambo ya kale nchini Syria wameonya juu ya majanga yanayosababishwa na kikundi cha wanamgambo wa dola ya kiislamu, Islamic State nchini humo baada ya kuukamata mji wa Palmyra, ambao ni miongoni mwa miji iliyotengwa kuwa uridhi wa dunia ulioko Mashariki ya Kati.

Wanamgambo hao wa IS wanaelezwa kukamata vijiji kadhaa vilivyo jirani na mji huo wa Palmyra na wamekwisha kuwaua wana vijiji zaidi ya ishirini wengi wao waliuawa kwa kukatwa vichwaa .

Mji huo wa Palmyra ni miongoni mwa miji inayohifadhiwa kutokana na historia yake nalo shirika la umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni ,UNESCO limekwisha kuutangaza mji huo kuwa hifadhi ya uridhi kwa dunia.

Kundi hilo la IS bila ya kujali wamekuwa waki haribu maeneo ya hifadhi za namna hiyo kama walivyo fanya nchini Iraq.

Palmyra nayo imekwisha kukabiliana na uharibifu huo wakati wa vita nchini Syria uliosababishwa na mgogoro wa kiraia dhidi ya serikali yao baada ya vikosi vya serikali kuweka kambi katika maeneo kama hayo ambayo ni urithi wa dunia.