IS latoa ukanda wa video wa Al Baghdad

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kiongozi wa kundi la Islamic state Al Baghdad

Kundi la Islamic State limetoa ujumbe kupitia mkanda wa video ambao linasema ulinaswa na kiongozi wake, Abu Bakr al-Baghdadi.

Hakujakuwa na uthibitisho wa hakika lakini wachambuzi wanasema kuwa sauti hiyo inafanana na yake.

Al-Baghdadi inasemekana alijeruhiwa vibaya mwezi Machi.

Lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa sauti hiyo haifanani ya mtu aliyedhohofika kiafya.

Ujumbe huo unazungumzia mashambulizi yaliyotekelezwa na jeshi la Saudia huko Yemen kuanzia machi ishirini na sita kumaanisha kuwa huenda kanda hiyo haijazidi wiki saba tangu irikodiwe.