Desmond Tutu amshtaki mjukuu wake

Haki miliki ya picha
Image caption Askofu mkuu mstaafu Desmond Tutu

Askofu mkuu mstaafu wa mji wa Capetown na mshindi wa tuzo la Nobel Desmond Tutu pamoja na mkewe wamemshtaki na mashtaka ya uhalifu mjukuu wao.

Katika taarifa kupitia wakfu wa Desmond na Leah Tutu hawakutoa maelezo zaidi ,lakini maafisa wa polisi wa Afrika kusini wamesema kuwa wanachunguza kesi kuhusu uharibifu wa mali kwa makusudi.

Mjukuu huyo Ziyanda Palesa Tutu anatarajiwa kujisalimisha kwa polisi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Desmond Tutu

Amesema kuwa amehuzunishwa sana.

Wakfu huo umesema kuwa familia imeshangazwa na kitendo hicho na wanatumai kwamba wataliweka nyuma swala hilo hivi karibuni.