Hali bado ni tete Burundi

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanajeshi wanne waliokuwa wamelazwa katika hospitali hiyo walichukuliwa na hadi sasa hatma yao haijulikani.

Maafisa wa usalama waaminifu kwa rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza wanaendelea na misako dhidi ya watu wanoshukiwa kuwa ''wasaliti'' mjini bujumbura.

BBC ina ushahidi wa uvamizi uliondeshwa na polisi nchini Burundi kufuatia jaribio la mapinduzi ambalo halikufaulu dhidi ya rais Pierre Nkurunziza jumatano iliyopita.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Misako inaendelea kuwatafuta maafisa waliohusika na Mapinduzi

Daktari kwenye hospitali moja mjini Bujumbura ameiambia BBC kuwa polisi watiifu kwa rais Nkurunziza waliwasili kwenye hospitali hiyo siku ya ijumaa

na kufyatua risasi kwenye chumba ambacho wanajeshi na raia waliokuwa wamejeruhiwa katika makabiliano ya siku ya ''Mapinduzi'' walikuwa wakipewa matibabu.

Mfanyikazi mwengine wa hospitali hiyo alisema kuwa wafanyikazi wenzake walishikwa na hofu na wakakimbilia usalama wao.

Image caption Rais Nkurunzinza alipokelewa kwa vifijo na nderemo aliporejea Bujumbura

Wanajeshi wanne waliokuwa wamelazwa katika hospitali hiyo walichukuliwa na hadi sasa hatma yao haijulikani.

Mapema ijumaa watu 18 wanaoshukiwa kupanga ''mapinduzi'' hayo, walifikishwa mahakamani lakini kiongozi wao mkuu meja jenerali Godefroid Niyombare hajulikani aliko.

Hapo jana rais Nkurunziza aliwapongeza wanajeshi waaminifu kwa uadilifu wao na ukakamavu uliowawezesha kudhibiti ''wasaliti'' waliokuwa wametangaza ''Mapinduzi'' na kutaka kutibua vita na umwagikaji wa damu nchini humo.

Haki miliki ya picha AFP GETTY
Image caption Hali bado ni tete Burundi

Wale waliofikishwa Mahakamani ni pamoja na aliyekuwa waziri wa usalama Jenerali Cyrille Ndayirukiye na kamishna wa polisi Zenon Ndabaneze na Hermenegilde Nimenya.

Wakili mmoja aliyekuwa mahakani Anatole Miburo, ameiambia shirika la habari la AFP kuwa walishtakiwa kwa kujaribu kupindua serikali halali.

Bwana Miburo alisema kuwa walikuwa wamepigwa sana hasa Jenerali Ndayirukiye.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano bado yanaendelea katika sehemu kadha mjini Bujumbura

Jamaa zao walisema kuwa walikuwa wamepigwa sana na hata kupoteza uwezo wa kusikia kutokana na kipigo.

Mwandishi wa BBC aliyeko huko Karen Allen amesema kuwa maafisa wa jeshi wanne waliburutwa kutoka hospitalini walipokuwa wakipokea matibabu mmoja wao aliaga dunia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Hali bado ni tete Burundi

Hali ya usalama ilizorota nchini Burundi kuanzia tarehe 26 Aprili, rais Nkurunziza alipotangaza kuwa atawania awamu ya tatu katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi juni.

Wapinzani wake wanadai kuwa Nkurunzinza anakiuka mwafaka wa amani uliowekwa unaomruhusu rais kutawala kwa vipindi viwili pekee.

Watu 25 wamethibitishwa kufariki huku zaidi ya laki moja wakitorokea mataifa jirani wakihofu kutibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.