Fiji ndio mabingwa wa raga IRB 7s 2015

Image caption Fiji ndio mabingwa wa raga IRB 7s 2015

Timu ya raga ya Fiji ya wachezaji saba kila upande ndio mabingwa wa taji la msururu wa raga duniani wa wachezaji saba kila upande wa IRB, HSBC Sevens.

Fiji inayofunzwa na aliyekuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Uingereza ya raga ya wachezaji saba kila upande Ben Ryan ilinyanyua kombe hilo baada ya kuizaba Afrika Kusini 19-7 kwenye nusu fainali ya kombe kombe kuu iliyoandaliwa jijini London hii leo.

Mababe hao wa kisiwa cha pacific wanaotambulika kwa uhodari kwenye mchezo huo, walikusanya pointi za kutosha kwenye mkondo wa mwisho wa kombe hilo msimu huu na kumaliza wakiwa na jumla ya alama 147.

Afrika Kusini imemaliza katika nafasi ya pili ikiwa na alama 142.

Image caption Afrika Kusini imemaliza katika nafasi ya pili ikiwa na alama 142.

Fiji ilipewa taji hilo kufuatia ushindi wake dhidi ya Afrika Kusini kwenye robo fainali iliyochezwa Twickenham.

Savenaca Rawaca alifunga ''try'' mbili huku nahodha Osea Kolinisau akivuka mstari wa choka wa Afrika Kusini na kuipa Fiji taji lao la pili tangu mwaka wa 2006

Ufanisi wa Fiji umeifanya kuwa nchi ya pili baada ya New Zealand kushinda kombe la Sevens series tangu 2010.

"Ahsanteni sana kwa kuishabikia hii timu,".

Image caption Fiji imeibuka mshindi wa taji la dunia la msururu wa raga kwa wachezaji saba kila upande wa IRB, HSBC Sevens

Kolinisau aliiambia tovuti ya Raga duniani. ”Kuwa kikosi cha pili cha Fiji kushinda taji hili ni hisia kubwa”.

"Tunashukuru sana tumemaliza msururu huu, imekuwa ni safari ndefu,.

Timu za Fiji, Afrika kusini, New Zealand, na Uingereza, zimefuzu kwa mashindano ya raga ya Olimpiki kwa wachezaji saba yatakayofanyika Rio, Brazil

baada ya kuchukua nafasi nne za kwanza katika msururu wa raga duniani mwaka huu.

Mwenyeji Brazil atakamilisha oradha ya timu za raga zitakazoshiriki kwenye Olimpiki.