Kerry aitaka China kupunguza misukosuko

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption John Kerry

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry amezumgumzia misukosuko inayozidi kuongezeka kusini mwa bahari ya China alipokutanma na viongozi wa vyeo vya juu wa chama cha Kikomisti mjini Beijing.

Ameitaka China kuchukua hatua ili kupunguza misukosuko eneo hilo. Marekani inasema kuwa China imejenga miradi ya ardhi ya karibu ekari 800 kwenye visiwa vya Spratly mwaka mmoja uliopita.

Nazo meli za jeshi la marekani zimekuwa zikipiga doria kwenye visiwa vya spatry ambavyo vinadaiwa na china na nchi zingne tano.

China inaamini kuwa Marekani inazichochea nchi za Asia kukabiliana nayo katika kudai maeneo ya bahari.