IS wauteka mji wa Ramadi

Haki miliki ya picha ap
Image caption Wapiganaji wa Islamic State

Baada ya mapigano makali kwa siku kadhaa katika mji wa Ramadi nchini Iraq,hatimaye mji huo kwa sasa unashikiliwa na wapiganaji wa kundi la IS.

Makundi ya wanajeshi wa serikali wamekimbia kutoka katika eneo hilo na Islamic State wamejitangazia ushindi dhidi ya mji huo na kwamba wanaushikilia.

Mapema msemaji wa Gavana wa jimbo hilo amesema kuwa wapiganaji hao wanayashikilia baadhi ya majengo mhimu ya serikali katika jimbo hilo.

Hata hivyo umoja wa Mataifa umelaani hatua hiyo ya IS,ambapo pia Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi amesema kuwa kwa sasa wanajipanga kwa kushirikiana na majeshi ya Shia ili kukabiliana na wapiganaji hao.