Islamic State wasafirishwa kwenda Ulaya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wahamiaji wanaosafiri kwenda Ulaya

BBC imefahamishwa kuwa wanamgambo wa kundi la Islamic State wanasafirishwa kwenda barani Ulaya na walanguzi wa binadamu wanaohudumu kwenye bahari ya Mediterranean.

Mshauri wa serikali inanayotambuliwa kimataifa nchini Libya anasema kuwa walanguzi hao huwaficha wanamgambo ndani ya mashua zilizojaa wahamiaji.

Walanguzi wengine nchini Libya wanasema kuwa wanamgambo wa Islamic State huwaruhusu kuendelea na shughuli zao kwa malipo ya asilimia hamsini ya pesa wanazopata.

Mashirika ya mipaka barani ulaya mapema mwaka huu yalionya kuwa wapiganaji wa kigeni hutumia njia zisizokuwa za kawaida kuingia barani ulaya.