Taylor Swift ang'ara tuzo za Billboard

Image caption Taylor Swfit

Mwanamuziki nyota Taylor Swift ameshinda tuzo nyingi katika sherehe za tuzo za muziki za BillBoard baada ya kushinda nane kati ya 14 alizoteuliwa kugombea.

Miongoni mwa tuzo alizoshinda ni msanii bora wa kike,kanda bora ya video ya muziki wa ''Shake it off ''pamoja na msanii bora mwaka huu.

Nyota wa Uingereza Sam Smith alishinda tuzo la msanii mpya bora na kukubali tuzo lake akiwa nyumbani baada ya kufanyiwa upasuaji.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Taylor Swift

Lakini Kanye West alizomwa alipokuwa akifunga sherehe hiyo kwa kuimba mchanganyiko wa nyimbo zake.

Mashabiki wa muziki walimzoma huku mashemeji zake Kendall na Kylier Jenner wakizitaja nyimbo atakazoimba,huku mashabiki wakiendelea kumzoma.