Wavuvi waagizwa kutowasaidia wahamiaji

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji wa kabila la Rohingya waliookolewa na wavuvi

Wavuvi kutoka Indonesia wamesema kuwa wameamriwa na Serikali kuwa wasiwalete wahamiaji wanaopatikana wakielea kwenye vyombo baharini wasiokuwa na chakula au maji ya kutosha.

Maelfu ya wahamiaji wanadhaniwa kuwa wanaelea Baharini katika maeneo karibu na Indonesia, Thailand na Malaysia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Baadhi ya wahamiaji waliookolewa na wauvuvi Indonesia

Licha ya wito wa Umoja wa Mataifa kuwa wahamiaji waruhusiwe kufika ufuoni, mataifa hayo matatu yamefukuza boti zilizojaa wahamiaji.

Ni wale watu wanaojitahidi kufika nchi kavu pekee wanaoruhusiwa katika nchi hizo.

Haki miliki ya picha ap
Image caption wavuvi wa Indonesia

Wahamiaji wengi ni Waislamu wa jamii ya Rohingya wanaotoroka mateso nchini Mynamar.

Watu wengi wanataka taifa la Myanmar kuchukua wajibu mkubwa zaidi kuhusiana na wahamiaji hao lakini taifa hilo limekataa likidai kuwa halipaswi kulaumiwa kwa hali hiyo.