Mashua za wahamiaji kuharibiwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wahamiaji

Mawaziri wa nchi za muungano wa Ulaya wanakutana leo kuidhinisha mipango ya kuharibu mashua zinazotumiwa kusafirisha wahamiaji kwenda Ulaya kutoka nchini Libya.

Mara mipango hiyo itakapothibitishwa ujumbe wa muungano wa Ulaya utakusanya habari kuhusu shughuli za walanguzi wa binadamu na kulenga mashua zao baharini.

Viongozi wa Ulaya wanalenga kuchukua hatua kama hizo za kijeshi eneo la bahari la Libya na pwani ya Libya.

Karibu wahamiaji 6000 wanakadiriwa kuvuka bahari kutoka Afrika kaskazini na kuingia Ulaya mwaka huu.