Muuguzi awaua wagonjwa wake Uingereza

Image caption Muuguzi

Muuguzi mmoja amehukumiwa kwa makosa ya kuwaua wagonjwa wake wawili na kuwapa wengine 20 sumu katika hospitali ya Greater Manchester.

Victorino Chua alimuua Tracy Arden, mwenye umri wa miaka 44, na Derek Weaver mwenye umri wa miaka 83 katika hospitali ya Stepping Hill kwa kuwatilia sumu katika dawa zao.

Dawa zilizotiwa sumu zilitumiwa na wauguzi wengine ambao hawakujua mshtakiwa alikuwa ameyachafua.

Chua, mwenye umri wa miaka 49, aliondolewa kosa jingine la tatu la mauaji lakini akahukumiwa makosa mengine mengi dhidi ya wagonjwa wake kukiwemo mmoja ambapo mgonjwa alijeruhiwa ubongo wake.

Chua ambaye hakupatikana na kosa la kumuua Arnold Lancaster, mwenye umri wa miaka 81, lakini akapatikana na hatia ya kumwekea sumu kwenye dawa hakuonyesha hisia zo zote wake hukumu hiyo ilipokuwa ikitolewa. Atatangaziwa kifungo chake Jumanne.

Wagonjwa hao waliwekewa sumu kati ya Juni 2011 na Januari 2012.