Kipindupindu chawaua raia 15 wa Burundi

Image caption Wakimbizi wa Burundi

Wakimbizi 15 wa Burundi, wamefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu, baada ya kukimbilia usalama wao nchini Tanzania kwa mashua wakitokea nchini mwao Burundi.

Hayo ni kwa mujibu wa mashirika ya utoaji misaada.

Inasemekana kuwa wengine kadhaa wanaugua ugonjwa huo.

Shirika la Oxfam, linasema kuwa zaidi ya wakimbizi elfu sabini kutoka Burundi, wamefika katika rasi moja kisiwani nchini Tanzania, baada ya kutoroka ghasia za kisiasa nchini Burundi.

Kwa sasa wanahamishwa kwa mashua kutoka kisiwani humo, hadi nchi kavu.

Kuna upungufu mkubwa wa maji safi ya kunywa, chakula, makaazi na huduma za kimatibabu.