Maparomoko yawaua watu 50 Colombia

Haki miliki ya picha Direccin Nacional de Bomberos
Image caption Maporomoko nchini Colombia yawaua zaidi ya watu 50

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos anasema kuwa utawala wa nchi hiyo haujui ni watu wangapi ambao hawajulikani waliko kufuatia maparomoko makubwa ya ardhi ambayo yamewaua zaidi ya watu 50.

Waakazi wa mji wa magharibi wa Salgar wanasema kuwa nyumba wanakoishi watu maskini zilisombwa na matope pamoja na mawe kufuatia mvua kubwa iliyonyesha eneo hilo.

Makundi ya uokoaji yanatafuta kwenye vifusi kujaribu iwapo yatapata manusura.

Rais ameitaja hali hiyo kuwa janga la kitaifa na kusema kuwa atazijenga upya nyumba zilizoaharibiwa.