Saratani:Mwanaharakati ajifunga nyororo

Image caption david Ndung'u Wanjohi

Mwanaharakati David Ndung'u Wanjohi wa Ol Kalau kaunti ya mkoa wa kati nchini Kenya amejifunga nyororo katika chumba cha dharura cha hospitali kuu ya Kenyatta Jijini Nairobi na kuanza mgomo wa kutokula ili kupinga kile alichokitaja kama ukosefu wa vifaa vya kuwasaidia wagonjwa wengi wa ugonjwa wa saratani nchini.

Image caption Mwanaharakati aanza mgomo wa kutokula ili kuishinikiza jamii na serikali kununua vifaa zaidi vya tiba ya saratani

David ambaye ni baba wa watoto wawili amesema kuwa serikali na jamii kwa jumla inapaswa kutoa raslimali zilizopo kununua vifaa vya tiba kwa wagonjwa ambao wanangojea tiba hadi mwaka 2017.