China yapuuza dai la ujasusi wa kiuchumi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption China yapuuza madai ya ujasusi wa kiuchumi

Uchina imesema imesikitishwa sana na mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya raia wake sita na serikali ya Marekani kwa madai ya ujasusi wa kiuchumi.

Maafisa wa mashtaka wa Marekani wanadai kuwa wachina hao waliiba taarifa nyeti kutoka kwa kampuni za kiteknolojia za

Marekani zilizoko Silicon Valley ambako walikuwa wakifanya kazi ili kusaidia kampuni za Kichina kuwapiku kibiashara.

Washukiwa watatu kati yao ni Maprofesa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Marekani inadai wachina hao waliiba taarifa kutoka kwa kampuni za kiteknolojia za Silicon Valley

Profesa Hao Zhang alitiwa mbaroni mjini Los Angeles lakini wengine watatu wako nchini Uchina.

Waandishi wa habari wanasema kuwa Uchina mara kwa mara hupuuzilia mbali madai ya ujasusi lakini inaonekana kuwa dhana hiyo inaendelea kukubalika nchini Marekani.