Malaysia: Ulanguzi wa watu Asia wajadiliwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji huko Indonesia

Mawaziri wa mambo ya nje wa Thailand,Malaysia na Indonesia wanafanya mkutano wa dharura mjini Kuala Lumpur kujadili tatizo la wahamiaji haramu katika ukanda wao.

Nchi hizo tatu zinakabiliwa na shinikizo la kimataifa kuwasaidia maelfu ya wahamiaji waliokwama baharini.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wavuvi nchini Indonesia waliwaokoa zaidi ya wahamiaji 100 siku ya jumatano

Wahamiaji wengi ni waislamu wa jamii ya Rohingya waliokimbia kutoka Myanmar, lakini serikali ya nchi hiyo imekataa kuhudhuria mkutano huo.

Wavuvi nchini Indonesia waliwaokoa zaidi ya wahamiaji 100 siku ya jumatano

Haki miliki ya picha AP
Image caption Thailand,Malaysia na Indonesia zimekataa kuwaruhusu wamahiaji kuingia katika pwani za nchi zao

Bado kuna hofu kuhusu usalama na afya ya wale waliokwama baharini ambao wanahitaji chakula na maji.

Maelfu ya raia kutoka Bangladesh na Waislamu jamii ya Rohingya wamekuwa katika bahari ya Andaman kwa majuma kadhaa sasa baada ya serikali ya Indonesia kubadili sheria ilikukabiliana na walanguzi wa watu kupitia bahari na ardhi yake.

Thailand,Malaysia na Indonesia zimekataa kuwaruhusu wamahiaji kuingia katika pwani za nchi zao